English German

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi -- ambaye anamwakilisha Rais pia nchini Uswisi, Austria, Poland, Jamhuri ya Cheki, Slovakia, Romania, Bulgaria na Hungary -- aliwasilisha hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa Mh. Rais wa Ujerumani Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin hapo tarehe 06/06/2017.

akiondoka na rais baada ya kukabidhi hati
Mh. Balozi Dr. Abdallah Possi akiondoka pamoja na Mh. Rais wa Ujerumani Dr Frank-Walter Steinmeier kwa ajili ya kufanya mazungumzo mara baada ya kuwasilisha rasmi hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Read more ...

Uwezeshwaji wa vijana wenye vipaji maalumu

letterhead top embassy of tanzania in germany 2015t

Kwa Watanzania wote

KUKUSANYA MAONI KWA AJILI YA KUBORESHA MPANGO MAKAKATI WA KUWAWEZESHA VIJANA WENYE VIPAJI MAALUM

Ubalozi umepokea barua ya maombi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya kukusanya maoni ya “Disapora” ili kuandaa Mpango Mkakati wa kuwawezesha vijana wenye vipaji maalum kuwa chachu ya kuchangia maendeleo ya Taifa.

Ubalozi unaomba ufikishe ujumbe huu kwa Watanzania wote waishio Poland ili washiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi hili la kujaza madodoso ya Mkakati huu.

Read more ...

Kongamano la Diaspora 13-15 Agosti, 2015

letterhead top embassy of tanzania in germany 2015t

Kwa Watanzania wote

KONGAMANO LA DIASPORA (DIASPORA INVESTMENT CONFERENCE) KUANZIA TAREHE 13 HADI 15 AGOSTI, 2015, DAR ES SALAAM, TANZANIA

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu.

Ubalozi unapenda kukufahamisha kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhsirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu zinaandaa Kongamano la Diaspora (Diaspora Investment Conference) Dar es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti, 2015 katika hoteli ya Serena.

Read more ...

Kongamano la Biashara na Siku ya Mdahalo, 25-26/04/2014 Berlin

KARIBUNI WOTE

Kama mnavyofahamu kuwa siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza miaka hamsini (50), kwa lugha nyingine ni “Golden Jubilee”.

Katika kuadhimisha sherehe hii kubwa na muhimu, Ubalozi umeamua kuandaa Kongamano la Biashara (Investment Forum) kwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 pamoja na siku ya terehe 26 Aprili, 2014 kuwa siku ya mdahalo (Scholars' day) mjini Berlin, Ujerumani.

Madhumuni makubwa ya Kongamano hili ni kuwatangazia na kuwaonyesha umma wa Wajerumani mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya muungano wetu kwa kuwaonyesha fursa tulizonazo za biashara katika nyanja za kilimo, utalii, nishati na madani, viwanda, elimu n.k.

Read more ...

Text Size

Weather

77°
25°
°F°C
Scattered Thunderstorms
Humidity: 94%
11 kph
Sun
Thunderstorms
73 | 85
22 | 29
Mon
Thunderstorms
73 | 86
22 | 30